• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika kushirikiana kujenga Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa shughuli za kitamaduni

    (GMT+08:00) 2020-10-27 19:02:02

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China na Afrika zitatoa mchango wa kitamaduni kwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili, ili kuwafanya watu wa pande hizo kujenga uhusiano wa karibu zaidi, na kuanzisha kwa pamoja Jumuiya kati ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja kwa kufanya shughuli za kitamaduni.

    Huu ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na Jukwaa la tano kati ya vijana wa China na Afrika, ikiwa shughuli muhimu chini ya mfumo wa Baraza hilo limefunguliwa jana mjini Beijing.

    Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw. Wang amesema China na Afrika zitaendelea kutekeleza makubaliano ya mawasiliano ya utamaduni yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa viongozi wa FOCAC mwaka 2018, kuondoa athari mbaya zilizosababishwa na maambukizi ya virusi vya Corona, na kutafuta njia mpya za mawasiliano na ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako