• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini: Maendeleo ya miundombinu yatarajiwa kusaidia kufufua uchumi

    (GMT+08:00) 2020-10-28 09:05:58

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema miradi ya maendeleo ya miundombinu inatarajiwa kuchukua nafasi muhimu katika kukwamua uchumi wa nchi hiyo.

    Akiongea kwenye ufunguzi wa hoteli na kituo cha mikutano mashariki mwa Johannesburg, Rais Ramaphosa amesema mpango wa serikali unalenga kuhimiza maendeleo mapya ya miundombinu, hatua ambayo ni muhimu katika kuongeza nafasi za ajira. Pia ameeleza imani yake kuhusu ukuaji wa uchumi katika siku zijazo, licha ya kuwa kwa sasa uchumi wa nchi hiyo umeathiriwa vibaya kutokana na janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako