• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawakamata watu 42 kwa tuhuma za kushambulia polisi

    (GMT+08:00) 2020-10-28 09:06:21

    Inspekta Jenerali wa Polisi wa Tanzania Simon Sirro amesema watu 42 wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na mashambulizi dhidi ya polisi waliokuwa wanasimamia usambazaji wa masanduku ya kupigia kura katika Kisiwa cha Pemba, Zanzibar.

    Bw. Sirro amewaambia wanahabari kuwa makumi ya watu kisiwani huko waliyarushia mawe magari yaliyokuwa yanasafirisha masanduku ya kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, na maofisa wa polisi waliokuwa wanasindikiza magari hayo pia walishambuliwa. Ofisa huyo pia amesema hali ni tulivu kwa Tanzania bara, na watu wako tayari kupiga kura zao leo Jumatano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako