• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya wakubaliana kuendelea kuunga mkono juhudi za amani na usalama katika eneo la Sahel

    (GMT+08:00) 2020-10-28 09:14:18

    Kutokana na kuonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kudorora kwa amani na usalama katika eneo la Sahel, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya wamelaani mashambulizi yanayofanywa dhidi ya raia na wana usalama kwenye eneo hilo, wa kikanda na wa kimataifa.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa na baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika (AU-PSC) na kamati ya siasa na mambo ya usalama ya Umoja wa Ulaya (EU-PSC), inasema pande hizo mbili zimejadili hali ya eneo la Sahel, Sudan na Somalia.

    Pande hizo zimetambua kuwa kudodora kwa hali ya usalama kwenye eneo la Sahel, kunasababishwa zaidi na hali ya kukosekana kwa uwiano wa kiuchumi na kijamii, ugaidi na uhalifu wa kupangwa, hali ambazo pia zimefanya hali ya kibinadamu iwe mbaya.

    Pande hizo pia zimesisitiza kuwa zitaendelea kuunga mkono tume ya umoja wa mataifa nchini Mali (MINUSMA), kikosi cha pamoja cha eneo la Sahel G5, na kuendelea kushughulikia vyanzo halisi vya kudorora kwa hali ya eneo la Sahel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako