• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la mawaziri la Zambia lapitisha utekelezaji wa Makubaliano ya eneo la biashara huria la Afrika

    (GMT+08:00) 2020-10-28 09:14:38

    Baraza la mawaziri la Zambia limepitisha utekelezaji wa eneo la biashara huria la Afrika (AfCFTA).

    Msemaji mkuu wa serikali ya Zambia Bibi Dora Siliya amesema baraza hilo limepitisha utekelezaji huo kwenye kikao chake kilichofanyika Oktoka 26. Amesema hatua hiyo itaiwezesha Zambia kulifikia soko kubwa zaidi na kuratibu ushirikiano wa kibiashara na jumuiya za uchumi za kikanda barani Afrika.

    Makubaliano ya kuanzishwa kwa eneo la biashara huria barani Afrika yalipitishwa na Umoja wa Afrika mwezi Machi 2018, na yalianza kutekelezwa Mei 2019. Zambia ilisaini makubaliano hayo mwezi Februari 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako