• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yafikiria kutoa dhamana za serikali ili kuondoa pengo kwenye ukusanyaji wa fedha za ujenzi wa miundo mbinu

    (GMT+08:00) 2020-10-28 09:14:59

    Serikali ya Kenya inafikiria kutoa dhamana za serikali kwa raia wake wa diaspora ili kupunguza pengo lililopo sasa kwenye ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu.

    Mkurugenzi wa sera za usimamizi na mikakati wa soko la mitaji la Nairobi Bw. Lie Ombara, amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa dhamana hizo zinawalenga wakenya wanaoishi nje ya nchi ambao hutuma fedha nyumbani kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Amesema wakenya wa Diaspora wameonyesha nia ya kuwa sehemu juhudi za ufufuaji wa Kenya, kupitia kuchangia fedha kwenye miradi ya muda mrefu.

    Bw. OMbara amesema tayari serikali imeweka hatua za kutoa dhamana kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu na miradi ya uhifadhi wa mazingira zinazovutia kupitia motisha wa kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako