• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yatahadharisha kuhusu wimbi jipya la nzige wa jangwani nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2020-10-28 09:19:02

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetoa tahadhari juu ya wimbi jipya la nzige wa jangwani nchini Somalia, ambalo lnaleta tishio kubwa kwa usalama wa chakula.

    Katika ripoti yake mpya kuhusu hali ya nzige wa jangwani, FAO imesema nzige wengi zaidi wataonekana kusini mwa Somalia katika siku au wiki kadhaa zijazo. Ripoti imeeleza kuwa kuna makundi ya nzige wakubwa na wadogo kaskazini magharibi kati ya Boroma na Hargeisa, huku makundi ya wakubwa wanaozaliana yakiwa katika sehemu ya kaskazini mashariki na sehemu kati ya Mudug na Galgaduud.

    FAO imesema ingawa nchi husika zimejiandaa vizuri zaidi ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita, lakini shughuli za uchunguzi na udhibiti bado zinahitajika kuendelea kugundua na kupunguza uvamizi wa nzige kadiri iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako