• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Philadelphia amuua kwa riasi mwanaume mweusi

    (GMT+08:00) 2020-10-28 09:29:25

    Vurugu zimetokea baada ya polisi kumuua kwa risasi mwanaume mweusi mjini Philadelphia, Marekani jana alfajiri na kusababisha polisi 30 kujeruhiwa na makumi ya waandamanaji kukamatwa.

    Vyombo vya habari vya Marekani vimesema polisi wawili walimpiga risasi mwanaume mweusi mwenye umri wa miaka 27 aliyejulikana kwa jina la Walter Wallace ambaye alikuwa anainua kisu mtaani. Baba wa Bw. Wallace amesema, polisi walimpiga risasi mara kumi mtoto wake aliyekuwa na matatizo ya akili na alikuwa akitumia dawa. Meya wa mji huo Bw. Jim Kenney ameahidi kuchunguza tukio hilo kikamilifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako