• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yasema kufikia makubaliano ya kuridhisha kuhusu bwawa la Nile kunahitaji nia ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2020-10-28 09:39:53

    Wizara ya Umwagiliaji na Maji ya Sudan imetoa taarifa ikisema, kufikia makubaliano ya kuridhisha pande tatu kuhusu Bwawa la GERD kunahitaji nia ya kisiasa kutoka viongozi wa Sudan, Misri na Ethiopia.

    Mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri wa umwagiliaji wa Sudan, Misri na Ethiopia jana walifanya mkutano kwa njia ya video, ambapo walijadili kuanza tena kwa mazungumzo kuhusu bwawa la GERD chini ya upatanishi wa Afrika Kusini, ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika.

    Sudan imependekeza kuwapa nafasi kubwa zaidi wataalamu na wachunguzi kwenye mazungumzo ili kupunguza tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako