• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Air Tanzania yaanza tena safari zake kwenda Harare

    (GMT+08:00) 2020-10-28 16:54:41

    Safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (Air Tanzania) kuelekea mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, zimeanza tena baada ya kusitishwa kwa miezi saba kutokana na janga la mlipuko wa virusi vya Corona.

    Shirika hilo linaungana na mashirika mengine ya ndege ya kikanda na kimataifa yaliyoanza tena safari zake kwenda Zimbabwe baada ya nchi hiyo kufungua anga lake mwanzoni mwa mwezi huu.

    Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, kutokana na utaratibu mpya wa kawaida, safari hizo zitafanyika chini ya kanuni mpya za afya zinazolenga kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako