• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande mbalimbali zajiandaa na Maonesho ya CIIE yatakayofunguliwa hivi karibuni

    (GMT+08:00) 2020-10-28 16:56:18

    Maonesho ya tatu ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China (CIIE) yatafunguliwa hivi karibuni. Kutokana na hatua za kudumu za kukinga na kudhibiti virusi vya Corona, pande zinazohusika zinachukua hatua mbalimbali ili kuyaandaa kuwa maonesho yenye kiwango cha juu na ubora mzuri.

    Maonesho hayo yamegawanyika katika maeneo sita, ambayo ni vyakula na mazao ya kilimo, magari, teknolojia na mitambo, bidhaa za matumizi, mitambo ya matibabu na madawa pamoja na biashara ya huduma.

    Kutokana na janga la virusi vya Corona duniani, eneo la mitambo ya matibabu na madawa linafuatiliwa zaidi na watu, na kuyavutia mashirika 340 ya ndani na nje ya nchi kushiriki, yakiwemo mashirika zaidi ya 70 yanayoshika nafasi 500 za mwanzo duniani. Mkuu wa Ofisi ya ukuzaji wa uwekezaji kwenye Idara ya uagizaji biashara ya kimataifa ya China Cao Pei anasema:

    "Mwaka huu kutokana na janga la COVID-19 duniani, watu wanazingatia zaidi kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi na afya ya umma. Tumeanzisha eneo maalumu la mambo kama hayo kwenye eneo la mitambo ya matibabu na madawa. Hivi sasa makampuni mengi yanayoshika nafasi 500 za mwanzo yanashiriki kwenye eneo hilo"

    Kutokana na kanuni na hatua za kudumu za kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi, kabla ya kuingia kwenye maonesho, bidhaa zote zitapitishwa kwenye hatua ya kuua vijidudu na kuhakikisha usalama wa magari, wafanyakazi na bidhaa za maonesho. Msaidizi wa meneja mkuu wa Kituo cha Uendeshaji wa Kituo cha Maonesho na Mikutano cha Shanghai Peng Chunyan anasema:

    "Tunaua vijidudu kwenye ukumbi wa maonesho mara moja asubuhi, na mara moja usiku. Pia tunachukua hatua za kuua vijidudu katika vifurushi na kufanya upimaji wa nucleic acid kwa bidhaa mbichi zinazohifadhiwa kwenye mazingira ya baridi."

    Kabla ya kufunguliwa kwa maonesho hayo, idara mbalimbali pia zimechukua hatua mbalimbali katika kujiandaa kuhudumia maonesho hayo. Tarehe 27 Benki ya EXIM ya China imetangaza mpango maalumu wa utoaji wa huduma za fedha, na kupanga kutenga dola za kimarekani bilioni 52 katika kuagiza bidhaa. Wakati huo huo, mkurugenzi mkuu wa Idara ya usimamizi wa bandari kwenye Idara Kuu ya Forodha Bw. Wang Jun ameeleza kuwa, idara hiyo itatafuta njia mpya kuunga mkono biashara ya kielektroniki ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako