• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya waunga mkono Ngozi Okonjo-Iweala kuwa mkurugenzi mkuu wa WTO

    (GMT+08:00) 2020-10-28 16:56:57

    Uchaguzi wa mkurugenzi mpya wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) umeingia katika kipindi cha mwisho, na mmoja kati ya wagombea wawili, Bi. Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria na Bi. Yoo Myung-hee wa Korea Kusini atachaguliwa kuongoza Shirika hilo.

    Habari zinasema, mabalozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja huo wamethibitisha kuwa baada ya viongozi wa EU kujadili wiki iliyopita mjini Brussels, Umoja huo utamuunga mkono Bi. Ngozi Okonjo-Iweala kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa WTO.

    Umoja wa Ulaya umesema, uamuzi huo wa kuunga mkono Bi. Ngozi Okonjo-Iweala ni ishara kubwa ya kuimarisha utaratibu wa pande nyingi, pia unatoa ishara wazi na wa kuaminiana kwa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako