• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini ajitenga kutokana na kuwa karibu na mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-10-28 17:02:08

    Ikulu ya Afrika Kusini leo imetoa taarifa ikisema, rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa amejitenga kutokana na kuwa karibu na mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona, na kuongeza kuwa mpaka sasa rais huyo hajaonyesha dalili yoyote ya virusi hivyo.

    Taarifa inasema, Jumamosi iliyopita, rais Ramaphosa alihudhuria hafla ya ufadhili iliyozingatia mchakato wa kinga na udhibiti wa virusi vya Corona, na watu waliohudhuria hafla hiyo walivaa barakoa na kuwa na umbali wa kijamii. Lakini rais Ramaphosa alivua barakoa wakati wa chakula na alipokuwa akihutubia.

    Taarifa inasema, siku moja baada ya hafla hiyo, mgeni mmoja alianza kuonyesha dalili ya virusi vya Corona, na matokeo ya vipimo yalionyesha kuwa amepata maambukizi.

    Taarifa inasema, rais Ramaphosa ameanza kujitenga na kufanya kazi kwa umbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako