• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa yamkabidhi mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda kwenye DenHaag nchini Uholanzi

    (GMT+08:00) 2020-10-28 17:56:19

    Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema, Jumatatu wiki hii ilimkabidhi mtuhumiwa anayehusiana na mauaji wa kimbari wa Rwanda FĂ©licien Kabuga kwa shirika husika mjini The Hague nchini Uholanzi.

    Taarifa iliyotolewa jana na Wizara hiyo imesema, hatua hiyo inatokana na uamuzi wa mfumo wa usimamizi wa kimataifa kuhusu kesi zilizobaki za Mahakama ya Jinai ya Umoja wa Mataifa.

    Habari zilisema kuwa, Kabuga mwenye umri wa miaka 84 alikuwa mfanyabiashara wa Rwanda, na katika miaka ya karibuni aliishi nchini Ufaransa akitumia kitambulisho feki. Katika kipindi cha mauaji ya kimbari ya Rwanda, Kabuga alichochea chuki kati ya makabila kwa kutumia radio yake binafsi, na alifadhili vitendo vya mauaji hayo. Kabuga alikamatwa mwezi Mei mwaka huu kwenye kitongoji cha Paris.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako