• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei ya Mahindi Imeshuka kwa miaka 2

    (GMT+08:00) 2020-10-28 18:16:35

    Bei ya mahindi imepungua sana wiki chache tu, baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuamuru wafanyabiashara kulipa Sh2,500 kwa begi la kilo 90

    Wafanyabiashara wanawalipa wakulima Sh1,700 kwa mfuko wa kilo 90 , bei ya chini zaidi katika miaka miwili iliyopita. Mwaka jana, begi la mahindi lenye kilo 90 lilikuwa likiuzwa kwa Sh2,000 kwa mtumiaji.

    Wakulima wameanza kuvuna zao kuu la msimu katika maeneo mengi ya ya bonde la Ufa huku zoezi likitarajiwa kufikia kilele mwezi ujao.

    hata hivyo wafanyabiashara wanalalamika kwamba mahindi ambayo wanapata kutoka kwa wakulima yana kiwango cha juu cha unyevu na watalazimika kupata gharama zaidi katika kukausha nafaka.

    Rais Uhuru Kenyatta mwezi uliopita aliagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa wakulima wanalipwa kima cha chini cha Sh2,500 kwa mfuko kwa mahindi yao.

    Kenyatta pia ametoa maagizo mengine kadhaa yaliyolenga kulinda wakulima na kuongeza mapato yao, ambayo ni pamoja na kupunguza ada ya kukausha na kuhifadhi katika Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako