• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi Okonjo-Iweala apendekezwa kuwa mkuu mpya wa WTO, upinzani wa Marekani waleta sintofahamu

    (GMT+08:00) 2020-10-29 08:53:27

    Msemaji wa Shirika la Biashara Duniani WTO Bw. Keith Rockwell amesema aliyekuwa waziri wa fedha wa Nigeria Bibi Ngozi Okonjo-Iweala amependekezwa kuwa mkurugenzi mpya wa Shirika hilo.

    Bw. Rockwell amesema mabalozi watatu wa nchi kubwa wanachama wa Shirika hilo, wamependekeza Bibi Ngozi kuwa mkuu mpya wa shirika hilo kwenye mkutano wa ndani, na kusema ana nafasi nzuri ya kupata uungaji mkono wa nchi wanachama. Hata hivyo mmoja wao kutoka Marekani amesema hawezi kumuunga mkono Bibi Ngozi, na ataendelea kumuunga mkono waziri wa biashara wa Korea Kusini Bibi Yoo Myung-hee.

    Hata hivyo Bw. Rockwell amesema hataki kusisitiza sana kuhusu msimamo wa Marekani kwa sasa, kwa kuwa inawezekana hiyo ni njia ya Marekani kutaka kujipatia manufaa zaidi kutokana na uteuzi wake. Uteuzi wa Bibi Ngozi unatarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano wa baraza kuu la WTO utakaofanyika Novemba 9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako