• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shule nchini Kenya kwenye hatihati baada ya walimu na wanafunzi kuambukizwa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-29 08:53:48

    Katibu Mkuu wa wizara ya elimu ya Kenya Bw Belio Kipsang amesema kufunguliwa kwa shule hivi karibuni kumekumbwa na pigo baada ya wizara ya elimu ya Kenya kutangaza kuwa walimu 33 na wanafunzi 17 wameambukizwa virusi vya Corona.

    Bw. Kipsang amesema shule 35 zimetangaza kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, lakini ameondoa uwezekano wa shule kufungwa. Amesema serikali ina wasiwasi kuhusu uwezekano wa COVID-19 kuleta madhara makubwa kwenye ufundishaji darasani, na kuwa usalama wa walimu na wanafunzi ni muhimu. Na sasa serikali inatafuta njia ya kuimarisha usalama wa walimu na wanafunzi, wakati kufungua shule kwa awamu kukiendelea.

    Kenya ilianza kufungua shule kwa awamu Oktoba 12 ili kuwawezesha wanafunzi wa mwaka wa mwisho kumaliza masomo na kujiandaa kwa mitihani mwanzoni mwa mwaka kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako