• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Nigeria lakataa kuwapiga risasi waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga ukatili wa polisi

    (GMT+08:00) 2020-10-29 08:54:11

    Taarifa iliyotolewa na jeshi la Nigeria imekanusha tuhuma kuwa wanajeshi waliwafyatulia risasi watu waliokuwa wanaandamana kwa amani mjini Lagos wiki iliyopita, wakitaka ukatili wa polisi nchini humo kukomeshwa. Tukio hilo linatajwa kutokea Oktoba 20 na kufanywa na watu waliokuwa wamevaa sare za jeshi.

    Kwenye taarifa hiyo jeshi limesema ingawa Divisheni yake ya 81 ilihusika kwenye kurudisha utaratibu mjini Lagos baada ya serikali kutangaza amri ya kutotoka nje, wanajeshi wake hawakufyatua risasi. Taarifa imesema tuhuma hizo si za kweli, hazina msingi na zinalenga kuleta vurugu.

    Jeshi limesema liliitwa na mamlaka za mji wa Lagos ili kurudisha utaratibu baada ya hali kuonekana kuwa na mwelekeo wa kasi wa kutokea vurugu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako