• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha China cha kwenda sayari ya Mars chafanyiwa marekebisho ya tatu ya obiti

    (GMT+08:00) 2020-10-29 09:09:52

    Chombo cha China cha kwenda sayari ya Mars Tianwen-1 kimefanyiwa marekebisho ya tatu ya obiti jana usiku.

    Shirika la Anga za Juu la China CNSA limesema chombo hicho kimesafiri kwa siku 97 kwenye anga ya juu na sasa kiko umbali wa kilomita milioni 44 kutoka duniani, na mifumo yote ya chombo hicho iko katika hali nzuri. Chombo hicho kinatarajiwa kuingia kwenye obiti ya kuzunguka sayari ya Mars mwezi Februari mwaka kesho, na kufanya uchunguzi wa miezi miwili mitatu kutoka obiti kuhusu maeneo ya kutua kabla ya kutua kwenye sayari hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako