• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu milioni 5.2 wanahitaji msaada nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2020-10-29 09:11:14

    Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA, imesema kutokana na mafuriko, maafa ya nzige, mapambano na mlipuko wa COVID-19, watu milioni 5.2 nchini Somalia wanahitaji misaada.

    OCHA pia imesema msukosuko wa hali ya kibinadamu nchini Somalia unaendelea kuwa mkali zaidi duniani, na Umoja wa Mataifa na washirika wake wametoa msaada kwa watu milioni 2.3 nchini humo mwaka huu.

    Hata hivyo OCHA imesema fedha zinazotolewa kwa kila sekta hazina uwiano, kwani zaidi ya nusu ya makundi yanayohitaji msaada yanapata chini ya asilimia 35 ya fedha zinazohitajika.

    Mpaka sasa asilimia 61 ya dola za kimarekani bilioni 1.01 zinazotakiwa kwa ajili ya mwitikio wa kukabiliana na hali ya kibinadamu nchini Somalia, yaani dola milioni 618, zimepatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako