• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya China na Afrika vimetoa mwito wa kuimarisha ushirikiano wakati wa janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-29 09:22:20

    Wajumbe kutoka vyombo vya habari vya China na nchi za Afrika Jumatano wametoa mwito wa kuimarisha ushirikiano ili kupinga kulifanya janga la COVID-19 liwe la kisiasa, na kuwachafua wengine kwa kutumia janga hilo.

    Wajumbe wamesema hayo kwenye mkutano wa mawasiliano ya wanahabari uliofanyika jana kwa njia ya video. Washiriki wa mkutano huo wamesema, vyombo vya habari vinapaswa kutangaza juhudi za China na nchi za Afrika katika kupambana na virusi na michango yao katika kufungua tena maendeleo ya uchumi na jamii kwenye nchi zinazoendelea baada ya mlipuko wa COVID-19.

    Wajumbe wa mkutano huo wamefikia maoni ya kuunga mkono siasa ya pande nyingi na mfumo wa usimamizi wa dunia unaoongozwa na Umoja wa Mataifa, pia wameunga mkono Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye mapambano dhidi ya COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako