• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yafukua kaburi lililozikwa wahanga elfu 5 wa mauaji ya kimbari

    (GMT+08:00) 2020-10-29 16:10:19

    Mamlaka ya Wilaya ya Gatsibo, mashariki mwa Rwanda kwa kushirikiana na wakazi wa wilaya hiyo ya Taasisi ya Ibuka wanashirikiana kwa pamoja kufukua kaburi moja lenye miili 2,000 ya watu waliouawa katika mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994.

    Meya wa Wilaya ya Gatsibo Richard Gasana ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kwa njia ya simu kuwa, zoezi la kufukua kaburi hilo lililogunduliwa katika kata ya Kiziguro lilianza Jumanne na linatarajiwa kuchukua karibu wiki tatu.

    Miili ya watu waliouawa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda inaendelea kugunduliwa katika sehemu mbalimbali nchini humo, ikiwa ni zaidi ya miongo miwili tangu mauaji hayo yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa ni Watutsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako