• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa kufungwa tena kwa wiki nne kutokana na mlipuko mpya wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-29 18:47:00

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametangaza kuwa, nchi hiyo itafungwa tena kuanzia kesho Ijumaa kwa mwezi mmoja ili kudhibiti mlipuko wa pili wa virusi vya Corona.

    Katika hotuba yake iliyorushwa kwa njia ya televisheni, rais Macron amesema virusi hivyo vinasambaa kwa kasi ambayo haikutarajiwa, na kuongeza kuwa wimbi la pili la mlipuko wa virusi hivyo litakuwa hatari zaidi ya ilivyokuwa awali.

    Rais Macron amesema, watu wataruhusiwa kutoka majumbani mwao kwenda kazini, kupata huduma za afya, kutoa msaada, kufanya manunuzi ama kufanya mazoezi ya kutembea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako