• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya 3 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China kufunguliwa tarehe 4 Novemba

    (GMT+08:00) 2020-10-29 19:30:07

    Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Bw. Gao Feng leo hapa Beijing ametangaza kuwa, Maonesho ya 3 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China yatafunguliwa tarehe 4 mwezi Novemba huko Shanghai, na rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kuhutubia ufunguzi huo kwa kupitia video.

    Habari nyingine zimesema, maonesho hayo yanajumuisha maeneo sita, ambayo ni vyakula na bidhaa za kilimo, magari, vifaa vya teknolojia, bidhaa za kutumia, mitambo ya matibabu na madawa, na biashara ya huduma. Pia mwaka huu, maeneo maalum manne yameongezwa na yanahusiana na afya ya umma, matumizi ya teknolojia za kisasa katika usafiri, uhifadhi wa mazingira na kubana matumizi ya nishati, pamoja na bidhaa za michezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako