• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni wapungua kufuatia janga la Covid-19

    (GMT+08:00) 2020-10-29 19:42:47

    Huenda Kenya ikashuhudia kushuka kwa kiwango kikubwa cha pesa ambacho wawekezaji wanaingiza ndani ya nchi katika miradi mipya na inayoendelea.

    Hali hii imeletwa na janga la Covid-19 lililosababisha makampuni mengi ya kigeni kupunguza uwekezaji kwa sababu ya hali ya kutokuwa na uhakika inayosababishwa na janga la Covid-19.

    Ripoti mpya iliyotolewa na Kongamano la Biashara na Maendeleo la Shirika la Umoja wa Mataifa (Unctad) inasema kuwa kutokana na kutokana na kutokuwa na uhakika unaosababiswha na Covid-19,makampuni mengi yamezuia pesa zao na kupunguza uwekezaji kwa zaidi ya nusu ya kwanza ya mwaka huu.

    Shirika hilo la Umoja Mataifa linasema mwenendo huu unatarajiwa kuendelea kwa muda uliosalia kabla mwaka kuisha huku uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni ukitarajiwa kupungua kwa asilimia 40.

    Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Kenya kuandikisha punguzo katika uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni baada ya kupungua kwa asilimia 23 mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako