• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuchangia uzoefu wake katika kazi ya kupunguza umaskini duniani

    (GMT+08:00) 2020-10-29 19:53:29

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, China inafanya juhudi katika kuchangia uzoefu wake katika mambo ya kupunguza umaskini duniani, na kuzisaidia nchi nyingine zinazoendelea kutimiza lengo hilo kwa vitendo halisi.

    Bw. Wang amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo.

    Akijibu swali kuhusu nchi nyingi zinazoendelea duniani kutarajia kuiga uzoefu wa China katika kupunguza umaskini, Wang ameeleza kuwa, China imejenga vituo 24 vya kielelezo vya kilimo barani Afrika, hatua ambayo imewanufaisha watu zaidi ya laki tano za huko. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya uchukuzi ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja", unakadiriwa kuwasaidia watu milioni 7.6 kuondokana na umaskini uliokithiri, na wengine milioni 32 kuondokana na umaskini wa kiwango cha katikati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako