• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM atoa mwito wa ushiriki wa wanawake kwenye michakato ya kutafuta amani

    (GMT+08:00) 2020-10-30 09:12:26

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa ushiriki wa maana na wenye ufanisi wa wanawake kwenye michakato ya amani.

    Akiongea kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake, amani na usalama, Bw. Guterres amesema ushirikishaji wa wanawake unapanua uwezekano wa kupatikana kwa amani, utulivu, mshikamano wa kijamii na maendeleo ya uchumi.

    Amesema usawa wa jinsia ni suala la madaraka, na sasa madaraka yamedhibitiwa na wanaume. Akitoa mfano Bw. Guterres amesema wanawake wanaongeza asilimia 7 tu ya nchi duniani, robo tatu ya wajumbe wa timu ya kupambana na virusi vya Corona ni wanaume, na maamuzi kuhusu amani na usalama duniani yanafanywa zaidi na wanaume.

    Bw. Guterres amesema hatua za muda kama kuweka nafasi maalum kwa ajili ya wanawake, zinaweza kuleta mabadiliko makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako