• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wana matumaini kuhusu mwelekeo wa China baada ya mapendekezo mapya kuhusu mpango wa maendeleo kupitishwa

    (GMT+08:00) 2020-10-30 09:13:12

    Wataalamu mbalimbali duniani wamepongeza mafanikio ya maendeleo ya China na kueleza matumaini yao kuwa China itakuwa na mafanikio zaidi, yatakayonufaisha kufufuka kwa uchumi wa dunia kutokana na madhara ya virusi vya Corona.

    Mkutano wa tano wa kamati kuu ya 19 ya chama cha kikomunisti cha China ulifungwa jana na kupitisha mapendekezo ya kamati kuu kuhusu mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano (2021-2025) kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na mipango ya muda mrefu kuelekea mwaka 2035.

    Mchumi mwandamizi wa Taasisi ya taifa ya utafiti wa uchumi-jamii ambayo ni jumuiya ya washauri bingwa ya London Bw. Mao Xuxin, amesema mapendekezo yaliyotolewa ni mpango wa maendeleo ya ongezeko la uchumi na maendeleo ya kijamii ya China kwa miaka ijayo.

    Mtaalamu katika taasisi ya Schiller ya Ufaransa Bibi Christine Bierre amesema Chin ilipata maendeleo makubwa katika mpango wake wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano, hasa kwenye upunguzaji wa umaskini na ushirikiano wa "ukanda mmoja, njia moja", kuonyesha ubora na ufanisi wa upangaji wa sera wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako