• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe aitaka nchi yake kujiandaa kwa msimu wa kilimo

    (GMT+08:00) 2020-10-30 09:15:49

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana Alhamis alitaka nchi yake ijiandae ipasavyo kwa msimu ujao wa kilimo, wakati mvua nzuri zinatarajiwa kunyesha nchini humo. Zimbabwe ilikumbwa na ukame katika msimu uliopita, ambao ulipunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mazao ya kilimo, ikiwemo mahindi na tumbaku.

    Akifungua maonesho ya 110 ya Kilimo ya Zimbabwe, Rais Mnangagwa amewahimiza wakulima na wadau kujiandaa vizuri na kusambaza pembejeo ili kuhakikisha mavuno kwa msimu ujao wa kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako