• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani iache kueneza uongo na kudhoofisha uhusiano

    (GMT+08:00) 2020-10-30 09:29:20

    China imewataka baadhi ya viongozi waandamizi wa Marekani waache kueneza uongo na kudhoofisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Msemaji wa wizara ya mambo ye nje ya China Bw. Wang Wenbin, amesema hayo baada ya taarifa iliyotolewa hivi karibuni na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo kuitaja jumuiya ya taifa ya muungano wa amani wa China (NACPU) kuwa ni ofisi ya kibalozi.

    Bw. Pompeo pia amesema Marekani itaacha kushiriki kwenye makubaliano kati ya serikali za nchi hizo mbili kuhusu kuanzisha baraza la magavana kati ya China na Marekani ili kuhamasisha ushirikiano katika ngazi za chini, kwa kuwa Chama cha urafiki kati ya China na nchi za nje kimejaribu kuwashawishi viongozi wa majimbo na wa ngazi za chini.

    Bw. Wang amesema taarifa ya Bw. Pompeo ni mbinu ya kisiasa yenye msingi wa ubaguzi wa kiitikadi na ni aina nyingine ya uongo usio na ushahidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako