• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa rais wa Zambia atoa mwito wa kuimarisha juhudi za kutokomeza ukatili dhidi ya watoto

    (GMT+08:00) 2020-10-30 09:40:14

    Makamu wa rais wa Zambia Bibi Inonge Wina ametoa mwito wa kuimarisha juhudi za kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.

    Bi. Wina amesema watoto wanahitaji mazingira salama na ya amani ili kukua na kuwa wanajamii wanaowajibika.

    Alipoendesha mazungumzo ya mawaziri kuhusu kutokomeza ukatili dhidi ya watoto, Bibi Wina amesema ni lazima kuimarisha juhudi za ulinzi, ili kuhakikisha Zambia inashiriki uzoefu bora kwenye kuanzisha vituo vya kupambana na ukatili dhidi ya watoto kwa haraka.

    Vilevile ameiagiza wizara inayoshughulikia mambo ya watoto kuhakikisha Mswada wa Sheria ya Watoto unawasilishwa bungeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako