• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati Kuu ya CPC yaanzisha mfumo mpya wa utoaji habari na kufanya mkutano wake wa kwanza na wanahabari

    (GMT+08:00) 2020-10-30 14:10:50

    Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano wake wa kwanza na wanahabari leo Ijumaa ili kutambulisha na kufafanua kanuni elekezi za kikao cha 5 cha Kamati kuu ya 19 ya CPC, hatua ambayo inaashiria kuanzishwa kwa mfumo wa utoaji wa habari wa kamati kuu ya CPC.

    Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya kamati kuu ya CPC na Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Baraza la Taifa Xu Lin, amesema kuanzishwa kwa mfumo wa utoaji habari ni utaratibu muhimu wa kitaasisi na uvumbuzi katika kushikilia na kuimarisha uongozi wa jumla wa chama pamoja na kuboresha uwezo wa chama kutawala. Pia mfumo huu umeanzishwa ili kukidhi mahitaji ya hali mpya, na mahitaji ya sasa ya ujamaa wenye umaalumu wa Kichina ambho umeingia kwenye zama mpya.

    Kikao cha 5 cha Kamati kuu ya 19 ya CPC kilimalizika jana Alhamis.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako