• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utungaji wa Mpango wa 14 wa Maendeleo wa Miaka Mitano ni utekelezaji wa demokrasia ya kijamaa nchini China

    (GMT+08:00) 2020-10-30 16:37:01

    Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa awamu ya 19 ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefungwa hapa Beijing, baada ya kujadili na kupitisha "Mapendekezo ya kutunga Mpango ya 15 ya Miaka Mitano ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii na Malengo ya Mwaka 2035". Naibu mkurugenzi wa ofisi ya Kamati ya Mambo ya Kifedha ya Kamati Kuu ya CPC Bw. Han Wenxiu amesema, utungaji wa Mpango huo ni utekelezaji wa demokrasia ya kijamaa nchini China.

    Tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango mwaka 1978, imetunga mipango ya maendeleo kila baada ya miaka mitano, na kabla ya kutungwa kwa mipango hiyo, Kamati Kuu ya CPC hutoa mapendekeo yanayotakiwa kufuatwa. Bw. Han anasema, ( sauti )

    "Rais Xi Jinping ametoa maelekezo muhimu, akiagiza kuunganisha maoni ya ngazi ya juu na mapendekezo ya raia, na kuhamasisha watu wa hali mbalimbali kutoa mapendekezo kwa njia mbalimbali. Kuanzia tarehe 16 hadi 29 Agosti, kazi ya kutunga Mpango ya 14 ya Miaka Mitano ilipata zaidi ya mapendekezo elfu moja kutoka kwenye mtandao wa Internet."

    Aidha, Bw. Han amesema, rais Xi pia ameagiza majopo ya washauri bingwa kufanya utafiti kuhusu mada 37 kuu za maendeleo kwa ajili ya kutunga mpango hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako