• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa BRICS asema Afrika itafaidika na maendeleo endelevu yaliyo jumuishi

    (GMT+08:00) 2020-10-30 16:41:49

    Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la BRICS kanda ya Afrika Kusini Bi. Busi Mabuza amesema, Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika zitafaidika katika maendeleo endelevu yaliyo jumuishi.

    Mabuza amesema, Jukwaa la Biashara la kundi la BRICS, lililomalizika jumatano wiki hii, lilijadili mafunzo yaliyopatikana kutokana na uzoefu wa washiriki kuelekea lengo la pamoja la maendeleo endelevu na jumuishi. Amesema mkutano huo umefanyika wakati wa utata mkubwa wa kiuchumi ambao umetokana na janga la virusi vya Corona.

    Baraza la Biashara la BRICS limetoa wito wa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya serikali, wafanyabiashara na mashirika ya kijamii ili kuhakikisha kuwa hakuna anayebaki nyuma katika ufufukaji baada ya janga la Corona.

    Kundi la BRICS linajumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, ambalo kwa pamoja linawakilisha asilimia 42 ya idadi ya watu duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako