• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Wanyama kuwania tuzo ya mchezaji mpya Amerika na Canada

    (GMT+08:00) 2020-10-30 16:55:54

    Nyota Victor Mugubi Wanyama anayechezea timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars na timu ya Montreal Impact, amewekwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo za Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS) katika msimu wake wa kwanza kwenye ligi hiyo ya timu 26. Wanyama ambaye alijiunga na Montreal Impact akitokea Tottenham Hotspur nchini Uingereza Machi 3, 2020, amechaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji mpya wa MLS. Wanyama pia amewekwa kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya mtendaji wa wema katika jamii (MLS WORKS Humanitarian of the Year) ilio na watu wengine 25. Nchini Kenya, Wanyama pia ana wakfu unaolipia wanafunzi kadhaa karo ya shule na pia imesambaza vyakula, barakoa na viyeuzi wakati huu wa janga la virusi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako