• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mwamuzi Shomari Lawi afungiwa mwaka mmoja

    (GMT+08:00) 2020-10-30 16:56:50

    Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imekutana tarehe 27 Oktoba na kuoitia mwenendo wa matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi kadhaa. Miongoni mwa maamuzi hayo, mwamuzi Shomari Lawi amefungiwa kuchezesha soka kwa miezi 12 kwa kushindwa kuumudu mchezo namba 50 wa Tanzania Prisons FC na Simba aliochezesha Oktoba 22, 2020 katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa. Pia timu ya Tanzania Prisons imepigwa faini ya 500,000 kwa kosa la kuingiza magari ya viongozi na mashabiki wakati mechi ikiendelea. Kikao hicho pia kimetoza faini ya shilingi laki tano mchezaji wa timu ya SImba SC Bernard Morrison na kufungiwa kucheza mechi tatu baada ya kukutwa na kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Ruvu Shooting FC aitwaye Juma Nyoso.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako