• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 140 wafa maji wakijaribu kufika katika visiwa vya Canary kutokea Senegal

    (GMT+08:00) 2020-10-30 18:31:25

    Watu 140 wamekufa maji wiki iliyopita baada ya boti waliyopanda iliyokuwa na abiria karibu 200 kuzama katika pwani ya Senegal.

    Taarifa iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) imesema, ajali hiyo ni mbaya zaidi ya majini kwa mwaka huu wa 2020.

    Taarifa hiyo imesema, boti hiyo, ambayo iliondoka kwenye mji wa pwani wa Mbour nchini Senegal Oktoba 24 kuelekea visiwa vya Canary, Hispania, iliwaka moto saa chache baada ya kuanza safari, na kupinduka katika pwani ya mji wa Saint-Louis.

    Vyombo vya habari nchini Senegal vimesema, jeshi la majini la Senegal na Hispania pamoja na wavuvi katika maeneo ya karibu waliowaokoa watu 59 na kupata miili ya watu wengine 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako