• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema COVID-19 imechochea uvumbuzi wa mambo ya afya katika bara la Afrika

    (GMT+08:00) 2020-10-30 19:04:11

    Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema, vijana wa Afrika wameweza kuvumbua mambo mengi yaliyokabiliana na changamoto inayotokana na janga la virusi vya Corona.

    Katika taarifa yake iliyotolewa jijini Nairobi, Kenya hii leo, Mkurugenzi huyo amesema, virusi vya Corona ni moja ya changamoto kubwa za kiafya katika vizazi vingi, lakini pia ni fursa ya kuchochea uvumbuzi, ubunifu na ujasiriamali wa teknolojia za kuokoa maisha.

    Utafiti wa WHO umeashiria kuwa, zaidi ya uvumbuzi 120 wa afya umefanyika Afrika tangu janga hilo liliporipotiwa mapema mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako