• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya NMB yapata faida ya asilimia 76 robo tatu ya 2020

    (GMT+08:00) 2020-10-30 19:05:10

    Benki ya NMB imepata faida ya ongezeko la asilimia 76 la faida kabla ya kodi kwa kipindi kilichoishia Septemba 30, 2020.Kwa miaka mitano sasa, Tanzania imeshuhudia ukuaji imara wa uchumi uliowezeshwa na sera thabiti za kiuchumi za Serikali ya awamu ya Tano. Akitangaza matokeo ya robo ya tatu ya mwaka 2020 ya Benki hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema kuwa matokeo hayo yamesababishwa na kukua kwa haraka kwa uchumi wa Tanzania, sera wezeshi na mwendelezo wa ukuaji wa pato la taifa kwa miaka ya hivi karibuni kama ilivyodhihirishwa kwa nchi hiyo kuingia kwenye uchumi wa kati mwezi Julai mwaka 2020 na kwamba hayo yote yamesababisha sekta ya kibenki kufanya vizuri, ikiwemo Benki ya NMB. Aliongeza kuwa katika kipindi hiki, mkakati wa Benki ya NMB wa kukuza vyanzo vya mapato umejidhihirisha kwa ongezeko la mapato yatokanayo na uendeshaji kwa 14% kutoka bilioni 527 katika robo ya tatu mwaka 2019 hadi bilioni 600 katika robo ya tatu ya mwaka huu (2020). Alisema kuwa katika kipindi hiki programu za Benki za kudhibiti gharama za uendeshaji na matumizi ziliimarishwa na kusababisha uwiano mzuri wa gharama na mapato kwa 52%.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako