• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana wafaidika na kilimo cha mpunga Morogoro

    (GMT+08:00) 2020-10-30 19:05:50

    Watafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo nchini Tanzania (SUA) wamebaini kuwa kilimo biashara cha zao la mpunga kinacholimwa kwa wingi katika Bonde la Kilombero mkoani Morogoro, ndicho kinachowainua kiuchumi vijana wa eneo hilo.

    Prof. Ntengua Mdoe, alisema kupitia mradi wa Utafiti wa Sera za Kilimo Barani Afrika (APRA), wamebaini vijana wenye umri kati ya miaka 15-35 ambao ni sawa na asilimia 35.5 ya watu ndio wenye kunufaika zaidi katika bonde hilo.

    Alisema hayo wakati akiwasilisha utafiti wake kwenye warsha iliyoandaliwa na APRA.

    Alisema pamoja na kuonyesha ushiriki wa vijana kwenye kilimo hicho, bado wanakabiliwa na vikwazo ikiwamo ukosefu wa mitaji na mashamba ya uhakika ya kuendeshea kilimo hicho wengi wao wamekuwa wakikodi.Hata hivyo, alisema katika mapendekezo ya utafiti huo wamezitaka halmashauri za wilaya na serikali kutenga ardhi ya kilimo kwa ajili ya vijana kama ambavyo imeelekezwa kwenye Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999 ili kuwaondolea changamoto na kusaidia Taifa kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga.

    Mapendekezo mengine ni kuwapo kwa njia sahihi ya kuwasaidia vijana hao mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya vijana pamoja na fedha zinazotolewa na halmashauri ya asilimia 10 kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambapo vijana wametengewa asilimia nne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako