• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya kutekeleza mkakati mpya ili kuepuka kufunga shughuli zote wakati wa wimbi la pili la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-30 19:24:49

    Mkutano usio rasmi wa kilele wa Umoja wa Ulaya umesema, ili kuepuka kufunga shughuli zote kutokana na wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona, Umoja huo unaweka matumaini yake katika kutambulisha mikakati mipya ya kupima na kufuatilia watu waliowasiliana kwa karibu na mtu aliyeambukizwa.

    Umoja huo umejikuta katika wimbi la pili la maambukizi, ambapo umeripoti ongezeko la kasi la maambukizi ya virusi vya Corona.

    Taarifa iliyotolewa na mkutano huo inasema, viongozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubali kwamba kupima na kufuatilia watu waliowasiliana kwa karibu na watu wenye virusi ni muhimu kwa kuzuia kuenea kwa virusi na kusaidia kudhibiti hali ya maambukizi, lakini njia ya kawaida ya kutambua, utekelezaji na matumizi ya vipimo vinavyotoa majibu haraka bado haijapatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako