• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 24-Oktoba 30)

    (GMT+08:00) 2020-10-30 20:54:24
    RASIMU YA KUBADILISHA KATIBA KENYA YAZINDULIWA

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, wamezindua rasimu ya mapendekezo ya kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo kwa lengo la kusitisha ghasia baada ya uchaguzi na masuala mengine ya kisiasa.

    Wakati wa hafla hiyo, naibu wa rais William Ruto alitaka mjadala mpana utakaowashirikisha raia wote wa Kenya kuhusu rasimu hiyo kabla ya kupitishwa.

    Rasimu hiyo inapendekeza kubuniwa nafasi ya rais, makamu wa rais, waziri mkuu na manaibu wake wawili watakaoteuliwa na rais, Pamoja na kiongozi wa upinzani.

    Mabadiliko hayo yanaunda nafasi ya kiongozi wa upinzani, ambaye atakuwa amemaliza katika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro cha urais.

    Viongozi walihudhuria hafla ya uzinduzi wa rasimu hiyo katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi walikuwa na mawazo tofauti kuhusu yaliyomo kwenye rasimu hiyo ya jopo la maridhiano.

    Naibu wa rais William Ruto, ambaye hotuba yake ilitatizwa mara kwa mara na baadhi ya wanasiasa waliokuwa katika hafla hiyo, alionyesha wasiwasi wake kuhusu mapendekezo ya kuundwa kwa baraza la polisi litakaloongozwa na waziri wa usalama, akisema kwamba hatua hiyo itakuwa ya kuingilia uhuru wa polisi.

    Ruto alisema ripoti hiyo haijajumuisha kila raia wa Kenya serikalini iwapo wote watakaochaguliwa na rais katika serikali wanaweza kutoka chama kilicho madarakani na iwapo kina idadi kubwa ya wabunge.

    Ruto vile vile alisema kwamba hatua ya kubadilisha tume ya uchaguzi haifai kwa sasa akisema kwamba vyama vichache vya kisiasa haviwezi kuchagua makamishina wa tume hiyo na waandae uchaguzi huru na haki.

    Rais Uhuru Kenyatta anaendelea kusisitiza kwamba ripoti hiyo maarufu BBI, itasuluhisha matatizo yanayoikumba Kenya na kwamba ni vizuri kwa raia kuipitisha kupitia kura ya maamuzi.

    Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, alisema kwamba hatua ya kuifanyia marekebisho katiba ya Kenya ni muhimu katika kukomesha ukabila uliokita mizizi nchini Kenya.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako