• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Ulaya zarejesha vizuizi baada ya maambukizi ya COVID-19 kuongezeka kwa kasi

    (GMT+08:00) 2020-11-02 08:46:23

    Nchi za Ulaya zimelazimika kurejesha vizuizi ili kudhibiti mlipuko mpya wa virusi vya Corona unaotokea sasa katika bara hilo.

    Kansela wa Austria Sebastian Kurz ametangaza kuwa, nchi hiyo itaanza kutekeleza hatua za kudhibiti maambukizi kesho Jumanne hadi mwisho wa mwezi huu. Amesema vizuizi vya awamu hii ni tofauti na awamu ya kwanza, kwani maduka yataendelea kufunguliwa, ila ni lazima kudumisha umbali wa kijamii.

    Nchini Uingereza, waziri mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson ametangaza kuwa nchi hiyo itaanza kutekeleza vizuizi Alhamis wiki hii vitakavyodumu kwa mwezi mmoja. Hatua hiyo imekuja baada ya kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi kuzidi milioni moja.

    Ijumaa iliyopita, Ufaransa, ambayo ni kiini cha mlipuko wa virusi vya Corona barani Ulaya, imeanza kutekeleza vizuizi kwa kiwango kidogo, ambapo watu wanaruhusiwa kwenda kazini, kupata huduma za afya za dharura, mahitaji ya lazima ya familia ama kufanya mazoezi karibu na makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako