• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yasema COVID-19 na uvamizi wa nzige wa jangwani yaifanya taasisi hiyo kubadilika

    (GMT+08:00) 2020-11-02 08:46:48

    Mfululizo wa majanga yanayoliathiri eneo la Afrika Mashariki, hususan janga la virusi vya Corona, uvamizi wa nzige wa jangwani na mafuriko, vinalifanya Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) kubadilika kwa kasi kuliko ilivyokuwa awali.

    Katika taarifa yake, Katibu mkuu wa IGAD, Workneh Gebeyehu amesisitiza kuwa Shirika hilo linajitahidi kudhibiti athari hasi za kiafya na majanga ya kiasili katika kanda hiyo. Amesema huu umekuwa ni mwaka wa kujifunza, kubadilika na kufuata njia mpya za kufanya kazi, na kuboresha majibu ya kukabiliana na matishio mengi.

    Akizungumza kwenye mkutano wa kutunga mpango wa kimkakati wa miaka mitano wa IGAD, Bw. Gebeyehu amesisitiza umuhimu wa mawasiliano, ushirikiano na uratibu katika kutunga mkakati huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako