• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Sudan na Ethiopia watembelea bustani ya viwanda iliyojengwa na China

    (GMT+08:00) 2020-11-02 09:08:24

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed na mwenyekiti wa Baraza la Utawala nchini Sudan Abdel Fattah Al-Burhan jana wametembelea bustani ya viwanda ya Adama pamoja na eneo la viwanda la mashariki.

    Kwa mujibu wa ofisi ya waziri mkuu wa Ethiopia, viongozi hao wawili walifuatilia uzalishaji wa barakoa ya kukinga virusi vya Corona wakati wa ziara yao ndani ya bustani hiyo.

    Katika eneo la viwanda la mashariki, viongozi wametazama utengenezaji wa dawa na oksijeni unaofanywa na viwanda vya madawa vya China.

    Bustani hiyo iliyojengwa na kampuni ya CCECC ya China, ni sehemu ya mpango mkubwa wa serikali ya Ethiopia unaotaka kubadilisha uchumi wake wa kilimo kuwa wa kiviwanda ifikapo mwaka 2025.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako