• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa Kenya asema mshikamano kati ya China na Afrika ni muhimu kwa mapambano dhidi ya COVID-19 duniani

    (GMT+08:00) 2020-11-02 09:27:49

    Ofisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya sera za Afrika nchini Kenya Bw. Peter Kagwanja jana amesema, mshikamano kati ya China na Afrika ni muhimu kwa mapambano dhidi ya COVID-19 duniani.

    Katika makala yake iliyochapishwa jana kwenye gazeti la Sunday Nation, Bw. Kagwanja amesema ukanda wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) lenye asilimia 35 ya idadi ya watu duniani, ni eneo kubwa zaidi la mshikamano dhidi ya janga la COVID-19.

    Ameongeza kuwa eneo hilo linatoa mchango mkubwa kwa juhudi za dunia katika kuzisaidia nchi masikini zaidi kuepuka janga la COVID-19.

    Vilevile amesema, FOCAC inatoa mfumo mzuri kwa utandawazi wa viwanda barani Afrika ili kuongeza uwezo wa kukabiliana na magonjwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako