• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TUZO: Eliud Kipchoge na Janet Wanja washinda tuzo za Couture Africa Style

    (GMT+08:00) 2020-11-02 16:34:24

    Mwanariadha Eliud Kipchoge na mwanavoliboli Janet Wanja wameshinda vitengo vya wanamichezo maridadi kwenye tuzo za Couture Africa Style jijini Nairobi juzi Jumamosi. Katika tuzo hizo zilizofanyika kwenye hoteli ya Emara Ole Sereni, mshika rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 42 ya wanaume Kipchoge aliwalemea wanariadha George Manangoi na David Rudisha, wanasoka McDonald Mariga na Ronald Okoth na mchezaji wa raga Billy Odhiambo katika kitengo cha wanaume. Bingwa huyo wa Olimpiki, ambaye majuzi alimaliza mbio za London Marathon katika nafasi ya nane nchini Uingereza, anajivunia kuwa mtu wa kwanza kukamilisha mbio za kilomita 42 chini ya saa mbili alipomaliza mbio maalum za INEOS1:59 Challenge kwa saa 1:59:40 mjini Vienna, Austria mwaka 2019. Kipchoge atasherehekea kufikisha umri wake 36 hapo Novemba 5. Wanja, 36, ambaye ni seta mahiri wa klabu ya Kenya Pipeline na timu ya taifa ya Malkia Strikers, aliwabwaga Naomi Wafula (gofu), Sabrina Simader (kuteleza kwa ubao thelujini), Emily Muteti (uogeleaji), Evelyn Okinyi (mtunishaji misuli) na Hellen Obiri (mwanariadha) katika kitengo cha wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako