• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Mtanzania Twaha Kiduku amtwanga bondia Sorimongkhon Singwancha kutoka Thailand kwa TKO

    (GMT+08:00) 2020-11-02 16:34:42

    Bondia Mtanzania, Twaha Kiduku amemtwanga bondia Sorimongkhon Singwancha kutoka Thailand kwa TKO raundi ya saba. Kiduku mkazi wa Morogoro aliibuka mbabe kwenye pambano hilo la WBC la uzito wa kilogramu 76 lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Sabasaba. Mthailand huyo alikubali yaishe raundi ya saba baada ya kushushiwa mvua ya makonde ya maana kutoka kwa Kiduku ambaye alionekana kuwa bora mwanzo hadi mwisho. Mwamuzi, Pendo Njao ambaye naye pia ana uwezo mkubwa wa kuzichapa akiwa ndani ya ulingo alimaliza pambano hilo raundi ya saba baada ya Mthailand huyo kudai kwamba hataweza kuendelea na balaa uwanjani kwa kuwa alipata maumivu ya bega la kushoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako