• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Cristiano Ronaldo apona COVID -19 na kurejea kwenye timu yake

    (GMT+08:00) 2020-11-02 16:35:21

    Uongozi wa Juventus umethibitisha kuwa nyota wao Cristiano Ronaldo kwa sasa tayari ameshapona COVID -19 baada ya kubainika na Virusi hivyo ambapo alikaa karantini kwa muda wa siku 19. Ronaldo akiwa karantini alikosa mechi nne ndani ya kikosi chake ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Barcelona ya mshikaji wake Lionel Messi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wakipoteza kwa kufungwa mabao 2-0. Staa huyo alibainika kupata maambukizi ya Corona akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Ureno Oktoba 13 mwezi uliopita. Kwa mujibu wa taarifa Cristiano Ronaldo alifanyiwa vipimo kwa mara nyingine na amebainika kwamba hana Virusi vya Corona, kwa sasa anarejea kwenye timu hivyo hatajitenga tena kama ilivyokuwa awali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako