• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Laptop yamuumbua kigogo Simba, ashikiliwa na jeshi la polisi

    (GMT+08:00) 2020-11-02 16:35:40

    Hali si shwari ndani ya Simba, kwani baada ya vigogo kadhaa kuondolewa kwenye nafasi mbalimbali, mwingine yamemkuta baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma mbalimbali. Kigogo anayeshikiliwa sasa ni Hashim Mbaga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo aliyeondolewa miezi michache iliyopita katika nafasi hiyo, mara baada ya kujiuzulu ghafla kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wao, Senzo Mazingisa aliyehamia Yanga kwa sasa. Taarifa ambazo zimethibitishwa na Kituo cha Polisi cha Oysterbay ni Mbaga amekamatwa tangu majuzi baada ya kushtakiwa na mabosi wa klabu hiyo. Habari kutoka ndani ya Simba, zinadai Mbaga anashikiliwa kwa tuhuma za kunaswa kwa mawasiliano kwenye Laptop yake yanayodaiwa ilikuwa ni hujuma dhidi ya timu yake hiyo iliyotoka kupoteza mechi mbili mfululizo Ligi Kuu Bara. Hatua ya kushikiliwa kwa Mbaga inakuja zikiwa zimepita siku chache tangu klabu hiyo kuwatimua watumishi wanne wakiwamo wawili wa Idara ya Habari, Ally Shantry 'Bob Chico' na Jacob Gamaly pamoja na meneja wa timu Patrick Rweyemamu na kocha wa makipa, Mharami 'Shilton' Mohammed.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako